 |
| Kazi ilianza kwakishindo sauti zikapazwa. |
JOHN LISU NA ALBAMU YA UKO WAPI
(CCC UPANGA ) LIVE SHOW
Ubora wa mandhari wa Live Recording pamoja na Itifaki ya Mtiririko wa
waimbaji ndio uliosahaulisha machungu ya Maelfu ya Wakazi wa Jiji la
Dar-es-Salaam, Morogoro, Pwani , Zanzibar na nchi jirani Kenya
waliochelewa kuingia ndani ya ukumbi wa CCC Upanga kufuatia utaratibu
mpya wa usalama wakati wa kuingia kwenye Live Recording ya “Uko Hapa” ya
Mwanamuziki John Lisu.
Katika Ukumbi wa CCC Upanga Mwanamuziki wa Injili John
Leonard Lisu ameandika historia kwa mara nyingine kwa kurekodi albam ya
pili ya DVD katika Ukumbi huo. Kabla ya John Lisu kupanda na Kuanza
kurekodi watumishi wengine wa utangulizi walianza kazi ya kusafisha njia
hiyo. Wanamuziki waliohudumu ni pamoja na Mbomby Johnson, Neema Gospel
Kwaya, Pastor Paul Safari, Paul Clement na Abedinego Hango.
John Lisu alipanda round ya kwanza na kurekodi nyimbo 12 mfululizo
ambapo katika nyimbo hizo 12 amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa Kenya
Timothy Kaberia, pia amemshirikisha Mwanamuziki bora wa Injili Barani
Afrika katika Ukanda wa Africa Mashariki Christina Shusho. Katika
Collable hilo la John Lisu na Christina Shusho lilikuwa la aina yake na
kukonga nyoyo za watu. Mwanamuziki John Lisu alirudi tena na kumalizia
kurekodi nyimbo 6 na kutengeneneza jumla ya nyimbo 18.
Angalia picha mambo yalivyokuwa kama ilivyowekwa na
Allanjofficial.blogspot.com
 |
| John Lisu akiwa na music director wake Fred Kilago au mwite Masanja, jamaa ni kichwa cha muziki Tanzania inajivunia naye. |
 |
| Fred akiwa na ubavu wa Ona mwite Tumaini. |
 |
| Pastor wa DPC Abel akiwa anafunguwa event kwa maombi. |
 |
| Jukwaa likipendeza na watu wakiwa wengi vijana wanakwambia nyomi. |
 |
| Bomby Johnson akiwa Kikazi zaidi siku ya Jana. |
 |
| Tumaini Ona akiwa natabasamu kali. |
 |
| Pastor Paul Safari akimtukuza Mungu. |
 |
| Christina Halai kulia akiwa sambamba na wenzake. |
 |
| Milio yenye kubembeleza mweeee! |
 |
| Hakika ilipendeza. |
 |
| Neema Gospel Live Choir kutoka AIC Chang'ombe wakimsifu Mungu. |
 |
Kijana wa GWT, Paul Clement akiimba Mpenzi wa karibu.
|
 |
| Katibu Mkuu wa TAG Pastor Ron Swai akifungua rasmi Live Recording ya John Lisu |
 |
| Ma MC wa tukio Godwin Gondwe kutoka IPP pamoja na Sam Sasali a.k.a bwana harusi mtarajiwa wakienda sawa. |
 |
| John Lisu akijiweka sawa kupanda jukwaani kuanza kazi huku mkewe akimwangalia. |
 |
| Makofiiiiiii kwa John Lisu akipanda jukwaani tafadhaliiiii |
 |
| Lisu akikimbia kuelekea jukwaani. |
 |
| Kazi ilianza kwakishindo sauti zikapazwa. |
 |
| Wee ilinoga sana. |
 |
| Christina Halai akienda sawa, Sasali ameandika huyu dada huyuuu, hapana shaka waliokuwepo jana mnajibu. |
 |
| Uncle jimmy the blogger akienda sawa na watu wengine kucheza na kumrudishia Mungu utukufu. |
 |
| Wanaume wakiwa kazini mwe |
 |
| Uweponi mwa BWANA kila goti litapigwa. |
 |
| Godwin akiwa uweponi. |
 |
| John Lisu na Timoth Kaberia toka Kenya wakiwa Kikazi zaidi |
 |
| John Lisu na kundi lake wakipiga picha ya pamoja baada ya kazi nzuri. Picha by Samuel Sasali na Fred Kilago. |
No comments:
Post a Comment